Artist: Webi
Song: Twamhitaji
Album: All I Can Say
Year: 2009
Producer: David 'Blackman'Muthami
Record Label: Blackman Entertainment
Ubeti
Nitakiri siku zote kwamba pendo lako ni la kudumu.
Hakuna wa kufana nawe uliyekuwa tangu siku za kale,
siku za kale…
Kipokeo Tangulizi
Mungu wa ajabu,
kimbilio langu,
Mweza yote na sifu.
Nakuinamia uliyenifia ni kwako utukufu.
Kipokeo
Yanibidi sibadili nyimbo hizi niwapashe habari.
Mhifadhi wa maisha anabisha awe kwetu mfariji..
Ubeti
Rafiki wa kila msimu kitachotutenganisha si kitu.
Yaliyonifadhaisha ninayakabidhi kwako hakika, hakika.
Kipokeo Tangulizi
Ninatumaini wema na fadhili zipo kwa kila siku.
Wanisimamia wanipigania, na siendi kuzimu
Kipokeo
Yanibidi sibadili nyimbo hizi niwapashe habari.
Mhifadhi wa maisha anabisha awe kwetu mfariji..
| < Prev | Next > |
|---|
