Artist: VBO MP
Song: Kura kwa Vijana
Album: Orezo Wangu ni Mwack
Year: 2009
Chorus (VBO MP)
Vijana tutasmama, ndio tutasmama,
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Kura ni kwa nani….? Kwa si vijana.
Vijana tutasmama, ndio tutasmama,
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Kura ni kwa nani….? Kwa si vijana.
Verse 1: VBO MP
Round hii tutasmama,
Wazee itabidii wamehama,
Watahema, tushasema,
Hatutarudia hii makosa tena,
Watatuchocha, hatutachocheka,
Tutacheka,tuwaache nje wakibweka,
Tutawafyeka, ka manyasi,
Tupunguze tumbo zao na makasi,
Wazi, vijana wameamka,
Vijana wamerauka,
Vijana wamechanuka,
Sioni tukiririma,
Tushawapima kilo zao hazitoshi,
Tuko wengi ka moshi,
Foleni ka gari ya moshi,
Kura si ya kuforci,
Vijana kwa kikosi,
Pamoja, kura kwa vijana.
Chorus (VBO MP)
Vijana tutasmama, ndio tutasmama,
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Kura ni kwa nani….? Kwa si vijana.
Vijana tutasmama, ndio tutasmama,
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Kura ni kwa nani….? Kwa si vijana.
Verse 2: VBO MP
Hawa mafala wataduwa,
Tumeamua round hii tutachukua,
Tutawastua round hii wataungua,
Smameni vijana tutawachagua,
Hatutachagua hawa mabuda wenye wameshadishi,
Kwa offisi ni mafisi na ganji za sisi,
Na si tukianza ubishi wanafyatua risasi,
Na uizi pia ni kazi kama hakuna kazi,
Vijana, pandeni hii ngazi,
Tujue pale waufichanga viazi,
Kwa mfuko zao na tumbo zao,
Wanafanya wakenya walale na ubao,
Ingawa mi nilianguka mao,
Ukiniiba ntakupata na hiyo mao,
Iko wapi land,mahindi,na thao za baro,
Title deed za hao, wanatuiba na mao.
Chorus (VBO MP)
Vijana tutasmama, ndio tutasmama,
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Kura ni kwa nani….? Kwa si vijana.
Vijana tutasmama, ndio tutasmama,
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Vijana tutasmama, ndio tutasmama
Kura ni kwa nani….? Kwa si vijana.
Beat stops/instrumentation
Nawaskia……. (Cheers)
Nawaskia……. (Cheers)
Shangilia……. (Cheers)
Kura ni kwa nani..? kwa si vijana.
SPEECH: VBO MP
Tusilale kwa kazi bana, hapa kazi iko kazi iko,
Vijana, round hii ni time yetu,tutasema mara ngapi,
Mayoung blood waingie,wamelemewa kutusaidia,
Si ndio tunajua mashida zetu bana,
Maviongozi wako kati yetu bana,
Pale umetulia sahi kuna kijana mjanja,
Muinueni 2012 ikifika,
Bora akuwe chini ya 50,
Miaka ni chini ya 50,
Tusichague juu 50 jo,
Ka uko 50 na juu retire,
hujatosheka kukula ganji ya wakenya nini,
rudi shambani, kalime na hizo degree zako,
pia si tuna ma degree na ma phd,
pia ma masterz,
na ukabila hatutaki hapa,kabila yako ni kijana,
kabila yangu ni kijana,kabila yetu ni kijana,
na si wote ni wakenya,tunaongea sheng,kiswahili ama ngoso,
hizo zingine hatuzimezo,tumeachia mabuda wetu waongee hizo,
najua wanatuskia,najua pia, watatusuka, hatutasukika,
watatuchocha, hatutachocheka,
hawasaidii wakenya tushawamezo,
vijana kaeni na mimi,tujipange pamoja,tujijenge pamoja
tujiinue pamoja,tujijue,
kapimwe ukimwi ujue hali yako manze,
mwisho manze ni tujiamini,na tuamini mungu moja,
Yehovah, Allah,Yahwe.kura kwa vijana,kaa na me, VBO MP.
| < Prev | Next > |
|---|
