Artist:Uncle Konias
Song:Merimela
Year:2011
Language:Kiswahili
VERSE 1 LYRICS:
Merimela kipenzi rafiki wa karibu tangu hapo zamani
tulipoanza shule nasi tukiwa watoto ulikuwa mpole
tena mwenye adabu msichana mrembo kila mara mshindi
sifa nazo urembo ukaenea kwote ukipita ni whispers
Merimela kipenzi rafiki wa karibu tangu hapo zamani
tulipoanza shule nasi tukiwa watoto ulikuwa mpole
tena mwenye adabu msichana mrembo kila mara mshindi
sifa nazo urembo ukaenea kwote ukipita ni whispers
VERSE 2 LYRICS:
Kwa darasa la saba kipenzi Merimela ukaanza geuka
machali mbalimbali ata nao walimu wakakufanya quencher
na wewe ukakubali ingilia mapenzi ya kiholelaholela
na we kuwashukia waliokuwa karibu wakukupa ushauri
Kwa darasa la saba kipenzi Merimela ukaanza geuka
machali mbalimbali ata nao walimu wakakufanya quencher
na wewe ukakubali ile mapenzi ya kiholela holela
na we kuwashukia waliokuwa karibu wakukupa ushauri
VERSE 3 LYRICS:
nami nikakuonya, chunga sana maisha
na we kashauriwa, badilisha mienendo
na we kapuuza, waenjoy maisha
tena ukakataa, unavunja mifupa
nami nikakuonya, chunga sana maisha
na we kashauriwa, badilisha mienendo
na we kapuuza, waenjoy maisha
tena ukakataa, unavunja mifupa
VERSE 4 LYRICS:
Ukakosa bahati mrembo Merimela ukakwachua mimba
ukazunguka kwote ukitaka mawaidha juu ya mimba mpenzi
nawe ukadanganywa toa kitu kidogo ukafanya abortion
bila kushauriwa njia gani salama ya kujilinda mrembo
Ukakosa bahati mrembo Merimela ukakwachua mimba
ukazunguka kwote ukitaka mawaidha juu ya mimba mpenzi
nawe ukadanganywa toa kitu kidogo ukafanya abortion
bila kushauriwa njia gani salama ya kujilinda mrembo
VERSE 5 LYRICS:
Ukaambiwa uchili, ukasema ni ndoto
utumie mipira, ukasema si tamu
basi panga uzazi, ukasema ni hectic
heri upate uokovu, ukakataa ni mapema
Ukaambiwa uchili, [chill please] ukakataa ni ndoto [that's a dream]
utumie mipira, [aah] ukasema si tamu [haina ladha]
basi panga uzazi, ukasema ni hectic [vipi?]
heri upate uokovu, ukakataa ni mapema [mambo bado, uokovu bado]
VERSE 6 LYRICS:
Kwa shule ya upili mwendo ni ule ule mapenzi kiholela
kila mwaka ni mimba, kila mwaka abortion, ikakuwa mtindo
ata chuo kikuu raha ikapanda, vunjavunja mifupa
wadosi na fukara ukaonja Merimela na mimba ni kawaida
ukakuwa ni dustbin, ya kutupa takataka
ATM mashini, kila kadi yaingia
ukakuwa daladala, kila mtu akupanda
ukakuwa ni dustbin, ya kutupa takataka
ATM mashini [aii], kila kadi yaingia
ukakuwa daladala, kila mtu akupanda [kila mtu]
VERSE 7 LYRICS:
Bado nakumbuka siku ulionialika kwa harusi Merimela
ukanielezea umekwisha hitimu na umepata mchumba
kama rafiki yako kanisisitizia nisikose kufika
kazi umeshapata na mshahara unapata na itakuwa sherehe
mimi kama rafiki, nikafika huko mapema [sana]
ilikuwa ni shereha [kubwa], ya vifisho na nderemo
nilikuwa ni maombi [Haleluyah], na zawadi teletele
kila uso ni furaha [hahaha], siku hiyo ya harusi
VERSE 8 LYRICS:
Sasa miaka mitano imepita Merimela hujapata mtoto
kila siku kelele kati yako na bwana, anataka mtoto
ata na wakuu zako wanapiga kelele, wanataka mtoto
furaha imekwisha imebaki huzuni, kila siku mawazo [majuto]
kwa waganga umeenda, hujapata mtoto
kwa maombi umeenda, hujapata mtoto
dakitari akasema, beba mimba huwezi
dakitari akasema, beba mimba huwezi [mfuko umeharibika]
na uchungu ya machungu [ai Mela], umepatwa na virusi
na uchungu ya machungu [ai Mela], umepatwa na virusi Mela mama
[Kama ungejua tu, ungetahadhari mapema
lakini usilie, bado unanafasi]
VERSE 9 LYRICS:
Usilie, usilie, Mela mama
Usilie Mela mama, usilie Mela mama
Usilie Mela mama, usilie Mela mama
Usilie Mela mama, usilie Mela mama
unanafasi ya kuishi usilie, Mela mama
fanya tizi, Mela mama
kula vizuri, Mela mama
kula vizuri, Mela mama
fanya tizi, Mela mama
meza madawa, Mela mama
tuliza roho, Mela mama
tuliza roho mama, Mela mama
This is a dedication to all the university students
from Arusha, Kampala mpaka Nairobi Kenya
Ata Maselo kwetu, Hi warembo
tahadharini
ladha ya ndoa ni mtoto, na ukianza kutoatoa, utalia baadae