Song: Kiswahili Kitam
Year: 2009
Chorus
mi nakupa utam, utam tam tam
kiswahili kitam, kitam tam tam
mistari mitam, mitam tam tam
furahia usijamu, furahia usijam,
Verse 1
nimechoka ndio tu nimetoka Lamu
lakini nipe karatasi na kalamu
nikuandikie vitamu
nitulize yako hamu
nichonge zako fahamu
nikuongezee ufahamu
ili vyema ufahamu
sitaki zako salamu
na usinipigie simu
na kwangu usikamu
juu utaniabudu ka sanamu
nikishaoa wako binamu
Verse 2
mistari zangu ni sumu
tena ni mingi humu
ka samaki kisumu
nazispit kwa ukarimu
nikikudiss usijamu
ukapatwa na wazimu
ukule pork na we ni muisilamu
tafadhali usinilaumu
enda kuwa imamu
juu hapa haujahitimu
kula popcorn na ndimu
ukitazama hii filamu
Verse 3
akili zangu ni timamu
ni wakati umetimu
wa kupanga hizi mofimu
na kufanya tarakimu
njaa yako kuikimu
ata ka una pumu
kwa miduu haunu njumu
mi ni mwana Eve si mwana Adamu
so nipe hilo jukumu
juu hiyo sio ngumu
na nimekuja hapa kudumu
sababu hii game si haramu.
Tags:
| < Prev | Next > |
|---|
