| 
A+ R A-

(2 votes, average 3.50 out of 5)

Ngoma Bila Nguo

" target="_blank">LISTEN TO 'NGOMA BILA NGUO'

Artist: Short But Tough Newton Karish
Song: Ngoma Bila Nguo
Language: Kiswahili


kuna siku sitasahau
tulikuwa tukicheza dansi
mwaka mpya Ongata Rongai
ilikuwa siku ya mateso
ngoma kubwa ilikuwa imejaa
kina mama, wazee na dotcom
ilikuwa saa nane ya usiku
nikaskia kila mtu lala chini

tukaamrishwa kila mtu atoe nguo
nguo zetu zote wakakusanya
na wakasema tusonge mbele na ngoma
nikaamrishwa nicheze Muthoni Kifagio

Muthoni nikiku-remember K.K natoka jasho
Muthoni nikiku-remember natiririkwa na machozi
nikikumbuka vile nilikuwa nimeku-keep kwangu
Nairobi kwa nyumba yangu na hukuwa wee unatosheka

wewe ni uselessi
wewe ni baselessi
Karish mwana Muembu sita-forgeti your behaviour

mzee mmoja alikuwa amebahatika
kutoa nguo akabaki na Godfather
na imagine alikuwa na kitambi
akikatika ilikuwa kama video
pesa zetu zote wakabeba
manguo zetu wakatutupia kwa sakafu
tulipoona majambazi wamekwenda
kila mtu aling'ang'ana kuvaa nguo yoyoote

yule mzee alikuwa na kitambi
alitafuta ya kuvaa akakosa
mwishowe alivaa biker
ilikuwa imebaki bila mwenyewe
hakuna mtu alipata nguo yake
kama mimi zile nilivaa
nilipofika kwa nyumba yangu
moja yazo haikuwa ya mwanaume

hako kanguo kangefanya tukosane
na bibi yangu
mama watoto
hako kanguo kangefanya tukosane
na bibi yangu
mama watoto
alikuwa ameleta shida sana
kwa sababu kananuka marashi
na akasema niwache kum-enjoy
ujanja wangu
umefika mwisho
nafikiria mwenye kuvaa biker
alikuwa na shida kuliko mimi
nafikiria mwenye kuvaa biker
kwa bibi yake alipata shida sana


Related lyrics

Comments (0)
Write comment
Your Contact Details:
Comment:
Read : 644 times
Ghafla!Lyrics (Kenya)