| 
A+ R A-

(1 vote, average 1.00 out of 5)

Safari Yangu

Artist: Saint Crooner
Song: Safari Yangu
Album: Ghetto Stress
Year: 2010
Producer: Long Chase
Record Label: Point 45 Records/Dub Studio (Austria)


Oh maisha, Ni safari,

Safari yangu, Maisha yangu,
Safari yangu, Mie masikini,
Safari yangu, Sauti yangu,
Safari yangu, Kenya yangu,

Kumekucha asubuhi naamka,
Naivaa kabuti yangu kwa haraka,
Sina kiamsha kinywa na ninatoka,
Kazi yangu wadharau ya taka taka,
Naelewa sina pesa si kosa langu,
Kuzaliwa maskini si kupenda kwangu,
Najaribu najikaza kisabuni,
Na imani siku moja nitafika,

Safari yangu, Maisha yangu,
Safari yangu, Mie masikini,
Safari yangu, Sauti yangu,
Safari yangu, Kenya yangu,

Kweli mie masikini na si utani,
Nyumba kuukuu ni ya mabati,
Kila mara kukinyesha niko mashakani,
Magonjwa ya baridi, Nina huzuni,
Nimetafuta kazi bila bahati,
Naitishwa cheti changu maofisini,
Shida nitoe wapi na sijasoma,
Imebaki tu imani na nitashinda,
Aaah!

Safari yangu, Maisha yangu,
Safari yangu, Mie masikini,
Safari yangu, Sauti yangu,
Safari yangu, Kenya yangu,

Naipenda nchi yangu nitailinda,
Kwa uwezo wangu wote niipiganie,
Nitoe na ushuru nijenge Kenya,
Na kazi zangu zote nizifanye vema,
Tuache ufisadi,
Tuache ukabila,
Tuache ubaguzi,
Twende twende wote,
Maendeleo!

Related lyrics

Comments (0)
Write comment
Your Contact Details:
Comment:
Read : 594 times
Ghafla!Lyrics (Kenya)