" target="_blank">
LISTEN TO 'KIFO'![]()
Artist: Remmy Ongala
Song: Kifo
Language: Kiswahili
kifo, kifo
kifo hakina huruma
kifo, kifo
kifo hakina huruma
kifo, kifo
ukitaka kujua ubaya wa kifo
pita hospitalini
utakuta wengine wanalia eeh
wengine hawana miguu tena
wengine wana vidonda
wengine wana vipele
wengine wana ukurutu
wengine wamezaa watoto wamekufa
shauri yako wewe kifo
kifo kwa nini unatusumbua
umedhaliwa shauri ya kuishi
ulimwengu bila watu sio ulimwengu tena kifo eeh
kifo, kifo
kifo hakina huruma
kifo, kifo
ulikuwa na baba yetu
ulikuwa tu unamtegemea
kifo umemchukua baba yetu
leo tunakwenda tunahangaika
hatuna mahala pa kulala
wakati baba alikuwa yuko
watu walikuwa chungu tele
leo baba hayuko tena
wengine wanatusimanga
wengine wanatufukuza
shauri yako wewe kifo wee
kifo, kifo
kifo hakina huruma
kifo, kifo
alikuwa na mpenzi wangu
alibahatika kwenda ng'ambo
na alikuwa anamsubiri kwa hamu
na amerudi Tanzania eeh
nimefunga mpingo na maisha
mtoto wa kwanza tumezaa
mtoto wa pili angali tumboni
kifo wamjua mke wangu eeh
mwanangu analia kila siku
baba mama yuko wapi
nashindwa la kusema
machozi yananitoka
shauri yako wewe kifo wee
kifo, kifo
kifo hakina huruma
kifo, kifo
kifo ni wa Mbaraka Mwinshehe
amekwenda Nairobi
kutafuta maisha ya baadaye
Mbaraka Mwinshehe alifahamika sana
katika ulimwengu wa mziki
hata Ujerumani wanapiga rekodi za Mbaraka Mwinshehe
hata akicheza Zaire Franco, Tabu Ley anajua Mbaraka Mwinshehe
kifo, kifo
kwa nini umetukatili
ungesubiri arudi Tanzania
tumwone sura ya mwisho
tumzike mwana wetu sisi mwenyewe
lakini kifo wee
kwa nini hauna huruma
kifo, kifo
kifo wee kifo
kifo ni wa Bobby
kifo ni wa Pierre Tito
kifo ni wa Anna Marie
kifo ni wa Papa Romere
kifo ni wa Lucy
kifo ni wa Mercy
kifo ni wa Mwabedi Kipande
kifo ni wa Salumu Abdalla
kifo ni wa Lubanga
kifo, kifo wee
kifo ni wa Likonze Wekala
kifo inaua hata kipofu eeh
kifo siku ya mwisho kweli walimwengu hatukupendi
kwa nini unatuuaua
kifo, kifo
kifo ni wa Lubaba
kifo ni wao kifo wee
kifo ni wa Chinyama Chiyasa
mlezi wa Makwinze
wamekuja wote pamoja kutoka kwao
kifo hataki watu wakipendana
umezoea kututenganisha
kifo wee kifo
kifo hakina huruma
kifo, kifo
kifo wee kifo
kwa nini haonekani
kifo amenificha wapi
ungalikuwa unaonekana
kifo ungalikuwa muungwana kifo
kifo ungalikuwa ooh kifo wee
sijui la kusema kifo wee
kifo tungekupa rushwa
kusudi tuishi milele
kifo, kifo
kifo hakina huruma
kifo, kifo
siku yangu ikifika eeh
kifo niarifu mapema
niage wanangu
niage familia yangu yote
pesa zangu nizigawanye
zimebaki ni zile mwenyewe
kifo nakusubiri kwangu
kifo nakwenda dukani Kariakor
nanunua shati jipya
tai mpya, koti jipya,
suruali mpya, soksi mpya
kiatu kipya
kifo ntanunua sanda yangu mwenyewe
kifo ntalipa watu wanichimbie kaburi yangu ningali hai
staki kuzikwa na mtu ntajizika mimi mwenyewe kwangu hakuna matata hakuna kilio hakuna kulaumu
kifo nakwenda province
nanunua crate ishirini za bia
mwarubaini kwa wingi
shibuku kwa wingi
negelua kwa wingi
wazuki kwa wingi
kipumu kwa wingi
haya kwa wasela
kifo ntafanya party
ntaita ndugu zangu wote
marafiki zangu wote
washikaji wangu wote
wasela wote
niwape wa mwisho
na bia yangu mkononi
kifo niambie
tukutane wapi
ata mimi nitaenda mwenyewe kwa miguu
sitakulaumu tena kifo wee
nimeacha msimamo nyuma yangu
kifo wee kifo
kifo hakina huruma
kifo, kifo
kifo hajui uzuri wako
kifo hajali ubonia wako
kifo hajali umwamba wako
kifo hajali cheo chako
mbele ya kifo hautambi
kifo ni kiboko yao
kifo, kifo
kifo ni kiboko yako
kifo, kifo
kifo ni kiboko yao
kifo, kifo
kifo hakina huruma
kifo, kifo
kifo hakina huruma
| Next > |
|---|
