" target="_blank">
LISTEN TO 'DODOMA'![]()
Artist: Rabbit Ft. Harry Kimani.
Song: Dodoma
Album: Tales Of Kaka Sungura
Intro
“ hii story ni sad yani lakini track ni ya Dj Loop,Rabbit na Harry Kimani,
Huu dem anaitwa Betty ametoka Dodoma sahii ikabidii mbaka nipige story yake.”
Verse 1 (Rabbit)
Alikuwa ametoka Dodoma amekuja Nairobi kusoma,
Hivyo ndiyo alinieleza siku ya kwanza mi kumwona,
Nilipigwa intro nikawa na mafikra za ki lover,
Mafikra za kisasa tukaswitch numbers,
Usiku kabla habari alikuwa simu ananipigia,
Mpango nao unapangwa vile kesho ntampitia,
Betty! Msichana wa kibongo mrembo
Ana umbi na macho, mwili pia anacho,
Kujuana kwetu ikawa ni issue,kutukalisha pamoja ilituleta karibu,
Ananieleza hakutembea vilabuni akiwa Dodoma,
Tukiwa Tao ni Seasons, na Westy Rezorus,
Alinishangaza na mafikra ati pesa si shida,
Lodging za kifahari,hoteli za nyota tano, gani hatukuingia?
Nilimtomasa kimapenzi vile inafaa,
Ye naye alinionyesha jinsi vile mume anakaa,
Chorus (Harry Kimani)
Betty,Betty mbona umeniacha,
Akilini ninazo picha zako,
Betty,Betty mbona umeniacha,
Akilini ninazo picha zako,
Betty,Betty
Verse 2 (Rabbit)
Hatuonani na marafiki, kila wakati ni Betty,
Sikuhizi sifanyi mziki, kisa maana Betty,
Nao ukafika wakati, wazazi huu ni Betty,
Wakati huu ungesaka kwa kamusi maana ya mapenzi
Ungepata jina zetu Rabbit na Betty,
Alitambua miondoko ya Hip Hop kila wakati aliucheza,
Kando ya radio kuna kanda ya Fid Q na Proffesa,
Jay Z, Nas,Tupac, Naughty by Nature,
Mafikra nayo yakanijia, kwa akili nikawa na fear,
Alimaliza semester kadhaa chuo kikuu Nairobi,
Za Dodoma Tanga,Mikocheni ndiyo story,
Yule alinipiga intro akawa rafiki yangu kwa Facebook,
Barua pepe ndiyo zake ati nichungane na Betty,
Nikimuuliza kwanini ati kunieleza hawezi,
Tuesday Betty alinitumia sms asubuhi kunieleza,
Tukutane stesheni exactly 12:30,
Chorus (Harry Kimani)
Betty,Betty mbona umeniacha,
Akilini ninazo picha zako,
Betty,Betty mbona umeniacha,
Akilini ninazo picha zako,
Betty,Betty
Verse 3 (Rabbit)
Nimefika 12:30 mi sioni Betty,
Na matrain zote zishaenda kwanza za Tz,
Numba yake ya Zain, nimejaribu haifanyi,
Ukweli yangu ndiyo huo, nabado siupati,
Nilitoka stesheni usiku ile tu kutoamini,
Nilielekea nyumbani kunasa majonzi,
Baada ya wiki moja nasoma gazetini
Kuwa mwizi mkubwa Bongo ameuwawa mikocheni,
Wengine walikimbia Betty hakufanikiwa,
Picha lake kubwa kwa gazeti limebandikwa,
The East African, Daily Nation walitoa uhondo,
Ile kutoamini akili karibu iende kombo,
Kabla aende uwizi aliniandikia barua,
Ata nimetioka posta sahii nimeuchukua,
Anasema ‘Rabbit sikupenda kwangu lakini nilikupenda - Betty’
sikupenda kwake, lakini alinipenda kwa thati
mpenzi wangu wa Dodoma,
Betty!
Chorus (Harry Kimani)
Betty,Betty mbona umeniacha,
Akilini ninazo picha zako,
Betty,Betty mbona umeniacha,
Akilini ninazo picha zako,
Betty,Betty
Outro (Rabbit)
hiyo ndiyo story yangu na Betty, for real,
Sahii kila Tuesday mimi huenda train steshen 12:30 sababu hiyo ndiyo memory
Niko nayo ya Betty, motto wa Dodoma. Betty jo! Namiss huyo dem.
TRUE STORY.
| Next > |
|---|
