Artist:Paul Mwai
Song:Omba
Year:2011
Language:Kiswahili
CHORUS LYRICS:
Kesha ukiomba
kesha ukiomba
maana adui naye
atafuta walio lala
ili awaangamize roho yangu usilale
VERSE 1 LYRICS:
majaribu na shida zimetusonga
shetani ajaribu kutuandama kila wakati
mwenzangu tusimame
imara kwa wokovu
tukeshe tukiomba
na yote tutashinda
CHORUS LYRICS:
Kesha ukiomba
kesha ukiomba
maana adui naye
atafuta walio lala
ili awaangamize roho yangu usilale
VERSE 2 LYRICS:
Wakristo tu wanyonge
wa mwili na wa roho
Twamwomba Mungu wetu usiku na mchana
Atupe nguvu Zake
tushinde yule mwovu
maana bila Yeye sisi hatutaweza
CHORUS LYRICS:
Kesha ukiomba
Kesha ukiomba
maana adui naye
atafuta walio lala
ili awaangamize roho yangu usilale
VERSE 3 LYRICS:
Shambani Gethsemane
Yesu Aliomba
Baba kiondoe kikombe cha machozi
maana sio mapenzi Yangu yatimizwe
bali mapenzi Yako Baba yatimizwe
Mungu Kampa nguvu kashinda majaribu
CHORUS LYRICS:
Kesha ukiomba
Kesha ukiomba
maana adui naye
atafuta walio lala
ili awaangamize roho yangu usilale
VERSE 4 LYRICS:
Kilio ninacho mimi ni kwa wale wameokoka
adui ameamua kamwe hatatuacha
aleta majaribu usiku na mchana
vijana nawaomba, wazee na watoto
tusimame imara, na yote tutashinda
CHORUS LYRICS:
Kesha ukiomba
Kesha ukiomba
maana adui naye
atafuta walio lala
ili awaangamize roho yangu usilale...
| Next > |
|---|
