Artist: Nonini ft. Naomi
Song: Waliotuacha
Year: 2004
Intro
ah, ah, Calif Records
yea, Nonini, eeh
kaeni chini na mskize
hii ni the best of Genge 2004
Clemo! Eeh
waonyeshe kile unaeza do na hiyo guitar
eeh!
twende, aha, yeah, ah, aha, ohoo, eeh, yea
tena, aha, mmhh, naskia mpaka kwa haga
kwa mara ya mwisho, ooh, ooh
yea, aha
Verse 1 (Nonini)
jama wacheni tu niwaulize swali moja eeh,
hii ngoma ni rap na pia tunabonga
ungepatiwa wish moja hii dunia ingekua nini
najua mamanzi wengi wange-wish kuamka bed moja na Nonini
lakini kuna vitu muhimu unafaa kwanza kuangalia eeh
ka Mungu hivi akulindie familia
au chali asifanye saa yote manzi yake kulia
na pia kutia bidii mpaka ukue na mali
mali mingi kila siku si we uamka na unaona siku ya pili
bila kuwa na ugonjwa yoyote ndani ya hiyo mwili
basi hiyo ndio mali mingi naeza wish maisha yangu
na nashukuru Mungu naeza shika jo hii kalamu
kuandika hii ngoma tamu kwa hii kitabu
kuna watu wengi walitaka kuona leo hawajaona
kuna watu wengi walitaka kuolewa hawajaolewa
kwa hivyo wee jua kila saa ukiwa kwa bar unalewa
kuna mtu yuko hospitali jo anakatikiwa na hewa
wee unapewa unapewa unapewa
ye alijaribu kushikilia hewa akalemewa
Chorus (Naomi)
maisha ni mafupi ndugu wangu
waonyeshe mapenzi uwapendao
Mola uwabariki waliotuacha
maisha ni mafupi ndugu wangu
waonyeshe mapenzi uwapendao
Mola uwabariki waliotuacha
Verse 2 (Nonini)
naskia kulia nikiskia sauti ya hiyo guitar
pia nakumbuka mathangu saa zingine vile huniita
jina ya marehemu brathangu jo mkubwa
alituacha kabla ata mimi jo sijakua mkubwa
kabla ata hii local watu hawajaanza ata kuskia
local? ah
kabla ata hii genge haijakubaliwa kabisa
ndio maana siku hizi ata siendangi kanisa
ile uchungu mi huskia nikimwona kwa picha
ile uoga mi huskia nikitembea bila ye kwa giza
jama mkiona saa zingine staki kucheka
msichukulie ati Nonini siku hizi anakulenga
ni vile tu nikicheka jo hiyo mcheko yangu
hutoka exactly tu ka ile ya brathangu, eeh
jamaa moja alikuwa mtu wa reggae damu
na-wish pia angekuwa hapa askize ngoma zangu
ingembamba kila siku kufungua gazeti anione hapo
akiasha TV aone ngoma ananipata ndani bado
ye ndio hunipa roho ya kuandika ngoma mambo bado
na hii verse wacha tu niimalize hapo yea
Chorus (Naomi)
maisha ni mafupi ndugu wangu
waonyeshe mapenzi uwapendao
Mola uwabariki waliotuacha
maisha ni mafupi ndugu wangu
waonyeshe mapenzi uwapendao
Mola uwabariki waliotuacha
Verse 3 (Nonini)
ni ngumu, ni ngumu kuandika hii verse ya tatu
sababu hii verse imededicatiwa watu watatu
Unplugged ya 2002 ndio naikumbuka kabisa
sabu nilipanda stage moja na marehemu E-Sir
ndamskiza kila siku na mabeste ndani ya gari
na forever ngoma zake Kenya jo zing'are
Wicky Mosh hata kaa mi na wewe hatukuwai gongana
najua siku moja Mungu akipenda tutapatana
aah, twende tukawake... ntakumbuka vitu poa sana juu yake
Birthday yangu F2 alikua na mimi anajua wapi
nilikua nam-respect sana juu ya kitu moja
alikuwa mabeste sana na sisi hata ka alikuwa Ogopa
jamaa kwa hivyo vile miaka jo zinasonga
msiwai sahau hawa watu jo mkichonga
mkisoma mkichoma na kila saa mkiwa pamoja jo mkibonga, aah
Bridge (Nonini & Naomi)
siku zimeenda na mi nateta
mobna aliendaa
tafadhali imba na mimi
bado nampenda tutakutana tenaa
Mungu akipendaa
usilie usilie cheka na mimi
siku zimeenda na mi na tetaa
mbona aliendaa
tafadhali imba na mimi
bado nampenda tutakutana tenaa
Mundu akipenda
usilie, usilie, cheka na mimi
| < Prev | Next > |
|---|
