| 
A+ R A-

(5 votes, average 3.60 out of 5)

Makmende Ameji-waste?

 

S
a hii story ya Makmende imekam na ime-die hivo tu. Na Just a Band bado ni ma-ordinary vile tu jina yao inasema.

Story ya Makmende ikianza tuliona vitisho mob jo! Mara ati ilikuwa vida ya fao Kenya kuenea haraka hivyo. Walikuwa wanaiita 'viral video', yaani ilikuwa ka virus ya comp vile ilikuwa inasambazwa! Hiyo ni sawa, fame walipata, lakini mkwanja nayo?



Kusema ukweli hata wakina Blinky wenyewe wamesema hawakuwa wanategea vida yao ku-hit vile ili-hit. Lakini bado vile tu ikakuwa obvious vile Makmende ilikuwa jina kubwa mtaani, walifaa ku-take advantage hiyo story iwadosishe jo! Unaeza imagine vile msanii wa kawa anakuwanga amesota mbaya, ungedhani wote wanakuwaga wanangojea kitu ka hii i-happen, lakini vile inakaa, hata hawajui kenye watafanya hiyo time yenyewe ikifika! Wee imagine tu kenye ingekuwa ime-happen ka Makmende ingekuwa kitu ya Kinaija ama ya S.A hivi. Mwenye angekuwa ame-do hiyo stuff angekuwa ameji-sort mbaya mbovu! Na niko surest juu ya hiyo story!

Nilikuwa nimetarajia Makmende akuwe ashaingizwa kwa ki-advert hivi ya Lucozade ama kitu ka hiyo jo! Kusema ukweli mi ningeona ile sura ya Makmende kwa chupa ya Lucozade ningekwachu hiyo something mara hiyo hiyo! Lakini Just a Band waliamua kwa press conference juzi ati Makmende hatawai tokea in public. Si hiyo basi inamaanisha Makmende atabaki tu kwa ile vida ya 'Ha-He'? Blunder mbaya!


Related lyrics

Comments (0)
Write comment
Your Contact Details:
Comment:
Read : 1060 times
Ghafla!Lyrics (Kenya)