Hapo mwanzo, radio ndio ilikuwa ile njia ya kuji-market vipoa ka ulikuwa na ngoma. Tangu enzi za kina Fadhili Williams hadi zile siku Nameless alikuwa anaimba Megarider, ngoma yako ingechezwa tu kwa radio, tungejua wee ni msanii ako serious.
Enzi za kina Fadhili Williams hata unge-survive na ma-live performance, halafu washikaji wako wanakujenga wakiambia mabeste wao story zako, lakini vile tuliendelea, ikawa lazima ngoma yako ichezwe kwa radiio, otherwise ungekaa bila exposure.
Alafu sa wadhii wakaanza story ya video. Nakumbuka vile Prezzo na Nazizi walitoa ile vida ya 'Let's Get Down' si ilistua watu! Wagenge hawakuwa washawai ona maringo za maana ka hizo za Prezzo. Hapo ndio nadhani wasanii waka-realise vile video inaweza kujenga career yako. Wengi wakaanza kukuwa serious na mavida zao, alafu pia bei ya ku-shoot vida ilishuka. Sa ilikuwa lazma ukuwe na vida ya ngoma yako, otherwise wasee wataona hauko serious.
Siku hizi sa kuna hii story ya net. Vile hizi ma-fibre optic zimekuja, speed ya net itakuwa wana, na Wakenya wengi wataweza ku-afford hiyo story. Pia ma-mobile companies wanajaribu ku-make sure wasee wapate net kwote Kenya. Hii inamaanisha nini kwa music industry? Kusema ukweli, mi nadhani itamaanisha net sa ndio itakuwa njia ya pawa ya wasanii kuji-market. Majuu tayari kuna wasee washatumia net kupenya kwa industry, na wame-hit mbaya mbovu. Fala ka Soulja Boy(umpende usimpende) alitumia YouTube kutoboa. Sean Kingston naye ali-hook up na producer wake J. R Rotem kutumia MySpace.
Kuna wasanii washa-notice potential ya net na washaanza ku-maximise kwa hiyo sector. Nonini ameshaweka effort noma sana kwa campaign yake online.Website yake, noninimusic.com ilikuwa poa tayari ikitokea, lakini huu msee huelewa vile net inakuwanga dynamic, asha-upgrade site yake tena. Isitoshe, Nons ashaunda network nzima ya ma-website ka Mtaa TV na Mtaa FM, zenye zinajaribu kusaidia wasanii wenzake kuji-market online.![]()
Ka hiyo story haijakubamba bado, basi pengine unafaa kucheki story ya Makmende. Just a Band walitumia power ya net ku-market vida ya 'Ha-He'. Waliweka vida noma YouTube alafu siku moja mbili hivi wasee ka 20 thao walikuwa washasambaziana ile ngoma, na ili-hit bila hata hustle mingi!
Time ka hii mnaweza kuwa mnafikiria"Sa huu msee ameongea mob, lakini hajatuambia exactly chenye tutado"
Vile mi sikuwangi mtu wa pang'ang'a mingi, wacha niku-show vile mi ninge-manage campaign yangu ya net ka ningekuwa msanii:![]()
Kwanza ningeji-promote kutumia hizi njaro:
- Upload video kwa YouTube
- Upload audio kuuzia hapo PewaHewa.com
- Weka lyrics hapa KenyanLyrics.com
- Weka profile/ biography hapo Wikipedia
- Fanya ma-interview na zile magazines ziko online, kama Haiya.co.ke, mwafrika.com, vibeweekly.com
Alafu ningeendeleza ma-promo kwa ma-social site hivi:
- Ningeundisha FaceBook profile, page na group. Alafu niweke ma-status updates kwa zote, nikionyesha mafans hizo vitu nimefanya hapo juu
- Ningeundisha profile hapo Twitter na ku-tweet juu ya zile mamboz nafanya online. Hapo Twitter ningeweka updates kadhaa zenye ni personal za kubamba mafans kiasi.
- Ningeundisha profile ya MySpace, na ku-update mafans wa kule majuu na ma-story zangu.
Kazi mob, sio? Uskatense. Kuna manjaro mob sana ya kufanya hii process yote ikuwe automatic.
Sa vile nishamada kuundisha campaign ya sare, sa ningetafuta ka-web designer hivi aniundishie site ya mine. Ile site ingekuwa na story ya life yangu, habari ya ma-shows zangu, alafu pia ingekuwa na ile part ya kuuza mziki yangu. Story ka hiyo inaweza kunisaidia sana kwanza zile siku nimesota jo, na sina ma-show!
| < Prev |
|---|
