Tulipokuwa shamba mi nawe,
mapenzi yetu yalizidi,
kukuleta mjini we mama,
nimefanya kosa.


Mwezi haujapita tangu tuje,
weshaanza vituko mama,
najua wazuzuka we mama,
na mambo ya mjini,

muulize mwenzio Kibena,
alivyoteseka wo wo oo,
ukivamia mji kwa pupa,
utakuja juta,


CHORUS:


ewe mpenzi wangu hayo yasikilize sana
yasije yakakukuta nawe kama dada Kibena

ewe mpenzi wangu hayo yasikilize sana
yasije yakakukute nawe kama dada Kibena

oyee mizuka oyee
oyee mizuka oyee

oyee mizuka oyee
oyee mizuka oyee...